Kutokana matatizo ya kiafya kuwa janga kubwa na unene kupita kiasi nyama nyeupe(white meat) hasa wakienyeji  zimependekezwa sana na uhitaji mkubwa unazidi kila kukicha.Popote penye uhitaji kuna biashara na faida kubwa mno.Biashara ya kuku wa kinyeji inatoa fursa ya wewe kujiajiri na kutoka, kuna njia nyingi za kuanzisha biashara ya kuku wa kienyeji lakini mimi nikiwa mjuzi na expert wa biashara  nakupa moja tu ngumu kuanza rahisi kuiendeleza .
DONDOO MUHIMU KUANZISHA BIASHARA YA KUKU WA KIENYEJI.
  1. HAkikisha una eneo la kutosha kujenga banda na sehemu ya wazi.
  2. Hakikisha unajenga banda imara na limeezekwa vizuri (fuata utaalamu wa kujenga kama kuna upepo upe kisogo)
  3. nunua mashine ya kuangulia mayai incubator(inauzwa kutokana na idadi ya mayai inayoangua)
  4. tafuta mayai yenye mbegu na tumia mashine kuangua
  5. tunza vifaranga vyako kwa utaalamu na kuku wa kienyeji wanahitaji sehemu ya wazi  yenye udongo hukua haraka.
  6. unaweza kuuza vifaranga kwa wafugaji wadogo ama kuwakuza mwenyewe.
  7. Hakikisha unapata mtaalamu wa mifugo kwa chajo na dawa za magonjwa mbalimbali
BIASHARA YOYOTE INA CHANGAMOTO NDOGONDOGO JIANDAE KUZIKABILI NA SI KUZIKIMBIA
tafuta soko la kuku wako na unaweza uza kwa jumla ama rejareja

KWA MASWALI UNAWEZA KUWASILIANA NASI KWENYE KIBOX CHINI USISAHAU KUUNGANA NASI KWA KUBOYA LIKE YA PAGE YENYE KICHWA MAWAZO YA KIBIASHARA