Mara nyingi, ni vizuri kuwaza kuwa kila zao unalozalisha unawezaje kuliboresha na kukupatia kipato zaidi. Wakulima wa karanga walio wengi wamezoea tu kulima na kuuza karanga mara baada ya kuvuna na kuwaacha wengine wasio wakulima wakifaidika zaidi kutokana na jasho lao.

Ni vizuri kutafuta na kujifunza njia mbalimbali zinazoweza kusaidia kuboresha uzalishaji wako na pato likawa la uhakika zaidi, ambapo badala ya kuuza karanga zikiwa mbichi. Unaweza kutengeneza siagi ya karanga ukauza ikiwa bidhaa kamili.
Namna ya kutengeneza siagi ya karanga “Peanut butter”
 • Chambua karanga kuhakikisha zote ni nzuri.
• Kaanga, menya na upepete.
• Pima uzito kisha saga mpaka ziwe laini.
• Andaa sukari, chumvi na mafuta ya alizeti.
• Mafuta yawe 20% ya uzito wa karanga, sukari 6% na chumvi 1.7%.
• Anza kuweka sukari na chumvi huku ukiongeza mafuta kidogo kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
• Bandika jikoni moto ukiwa kidogo kwa muda wa dakika kumi na tano.
• Baada ya muda huo weka kwenye vifungashio na kuweka nembo tayari kwa kupeleka sokoni.

Kama una mtaji mzuri unaweza kuanzisha  kiwanda na kufanikiwa zaidi kwa mashine za kusaga karanga na kutengeneza peanut butter zinauzwa kama 1.8milioni hivyo kuongeza uzalishaji kwa haraka.
mashine ya kutengeneza peanut butter


 Makala hii imehaririwa na 
Mkulima Mbunifu
S.L.P 14402
Arusha, Tanzania.
info@mkulimambunifu.org

Pia unaweza kuendelea kupata MAWAZO zaidi kwa kuLIKE facebook page yetu / kutoFOLLOW twitter /Kujiunga na huduma ya WHATSAPP