Utunzaji wa nywele ni kitu cha kila siku kwenye maisha yetu.Kwenye jamii yetu kila mtu anajali anavyoonekana.Nywele zinaongezea muonekano wa kuvutia.Kuanzia mtoto mpaka mtu mzima wanataka huduma ya kutunza nywele. Kama unaweza kuhesabu gharama ulizotumia kwa mwaka mzima kutunza nywele utashangaa kwa kiwango kikubwa.Biashara ya salon zipo kila mahali lakini leo tutajifunza jinsi gani unaweza kukabiliana na ushindani huo na kumiliki idadi kubwa ya wateja.

Kabla ya yote kwanini nakushawishi uanzishe biashara ya saloni.
  1. Biashara ya salon unaweza kutenga muda wakufanya huku ukiwa na shughuli nyingine labda jioni tu na weekend(part time job).
  2. Biashara hii unaweza kuiendesha ukiwa nyumbani.
  3. Biashara unaweza kuifanya na biashara nyingine kama kuuza bidhaa za nywele, mafuta ya nywele n.k.
  4. Hauhitaji kubuni bidhaa yako binafsi.
Jinsi ya kufanikiwa katika biashara ya salon.
  • Unatakiwa uwe na ujuzi mzuri wa salon.Kama wewe ni kinyozi ama msusi utakiwa uwe na utaalamu wa nywele hivyo utakiwa uwaone watu wenye uzoefu katika maswala haya.
  • Uwe na ukarimu kwa wateja.
  • Siku macho yako yawaangalie washindani wako.Unatakiwa kuwatawala washindani wako.Unatakiwa ujue mapungufu ya saloni zao na pia nini kinawaimarisha katika saloni zao na ndio utafaidika zaidi.
  • Huduma nzuri kwa wateja.
  • Chagua sehemu sahihi.Watu wenye hukosea kuchagua sehemu sahihi, Sehemu sahihi si sehemu isiyo na saloni tu bali sehemu yenye watu wengi na inafikika kwa urahisi.Sehemu yenye wapitaji wengi inayoonekana kwa urahisi.Kuanzisha biashara mpya sehemu isiyo na biashara kama yako ninaweza kuwa hatari ama faida.
Mahitaji.
Kabla ya kuanzisha biashara hii hakikisha una vitu vya msingi kama,
     Curlers
    Hair Brush
    Chana
    Hair Dryer
    Hair Rollers
    Hair Wand
    Hair Waver
    Mkasi
    Straighteners
    Vibanio
     Kioo
     Kiti
    TV kuburudisha  wateja
    Barber Chairs
  • Kumbuka vifaa vya biashara ya salon inategemea salon ni mahususa kwa jinsia gani.
Biashara nyingine unazoweza kuzifanya pamoja na hii ni:-
  1. Kupaka nywele rangi.(Hair Colouring)
  2. Shampooing.
  3. Kuuza mafuta ya nywele. 
Njia nyingine kuvutia wateja ni.
  1. Ukarimu kwa wateja.
  2. Usafi na huduma nzuri.
  3. Punguzo la bei kwa mwezi wa mwanzo. 
Bofya LIKE kwenye Facebook page yetu ./ Follow Twitter yetu kwa Mawazo zaidi