Chakula kikuu barani Afrika ni ugali.Kuna watu wanaamini kabisa hawawezi kuhisi kama watashiba isipokuwa wamekula ugali.Ugali unatokana na nafaka kama mahindi, mtama, muhogo n.k.Jiajiri kwa kununua nafaka mashambani na kusaga, kufungasha na kuuza sehemu mbalimbali.Kutokana maendeleo ya ushindani kampuni nyingi hufungasha mojakwamoja kama 1KG, 2KG, 5KG na 10KG kuepuka uchakachuaji.
Uuzaji
Hapa ndipo ushindani huanza kutokea lakini mara nyingi kilo moja ni 1000TSH(50KSH).Kupata faida nzuri ni vema kufuta nafaka mojakwamoja kwa wakulima mashambani.
N.B. Pia aina ya mahindi huvutia sana wateja kwa mfano unga unaotokana na mahindi ya njano huvutia sana wateja na hupendwa sana kama unaweza fanya kilimo cha mahindi ya njano mwenyewe na kusaga na kufungasha unga unakuwa na faida maradufu na biashara inaenda haraka.