Kama una ujuzi wa kutengeneza baga, basi una nafasi nzuri ya kujiajiri na kujipatia kipato kizuri.Hata kama hujui kutengeneza baga nafasi bado unayo, ujasiriamali si kujua kitu fulani tu Bali kujua na kukitumia kwa kuangalia mapungufu yaliyopo na kuzalisha fursa mpya hata kuiga ni ujasiriamali(kuiga na kuboresha na sio kuiga tu(REFER innovation)).Kwa nchi zetu hizi za afrika kuna nafsi nyingi za kujiajiri na kufanikiwa. Sehemu atayochagua kuweka Baga shop yako ni muhimu zaidi kufanikiwa.Kama utaweka Baga shop yako barabara isiyo na watembea kwa miguu, kwa kweli itakuwa ngumu kwako kuuza.Chagua sehemu wapitaji wengi utaona matokeo mazuri. Siri ya kufanikiwa kwa Baga Shop yako ipo kwenye baga unazouza.Kama huna ujuzi jifunze kwanza, aina za unga zinachangia pia na monjonjo mengine.Wateja wataongezeka kila siku.Watarudi watarudi na wataita wengine. Kuna vifaa vichache vya kununua kama Oven, mixer na Cream cheese containers . Pia kama una sehemu ya wazi unaweza kuwa na viti, meza, sahani na vikombe.