Biashara nyingi leo zinaendeshwa kwa matangazo.Kwa kweli hakuna kampuni au Biashara inayofanikiwa bila kujitangaza.Tangazo ni kitendo cha kujulisha umma/wateja huduma mpya, bidhaa mpya n.k.Ili biashara isonge mbele lazima kuwe na mkakati maalamu wa jinsi ya kuwafikia mtu mmojammoja.Watu wengi wameweza kufanikiwa tu kwa kuwa mawakala wa kuwatangazia watu bidhaa zao mfano mwanafunzi aliyeacha chuo kikuu na kuanzisha mtandao wa kijamii Facebook yeye ameingia si tu kwenye list ya Matajiri kumi marekani bali hata duniani kitu anachofanya ni kutangazia watu bidhaa zao kupitia mtandao wake wa facebook.
Unachotakiwa kufanya ile uanze biashara hii

  • uwezo mzuri wa kuandika
  • ujuzi wa elimu biashara angalau kwa cheti
  • ujuzi wa kuunganisha watu na wateja
  • Uwe na tovuti yako rasmi(Pata tovuti kwa bei nafuu wasiliana nasi)
  • ofisi ndogo
  • kumpyuta moja
  • simu inayopatikana muda wote
  • printer
  • Camera
  • Scanner
  • business card
* vifaa hivyo vinatumika kuzalisha tangazo la picha

Jinsi ya kufanya 
Utanza kwa kutembea wajasirimali wadogo na wa kati wanaozalisha bidhaa au huduma fulani na kuangalia bidhaa zao kwa makini.Kisha utawaeleza umuhimu wa kutangaza bidhaa zao na manufaa watakayopata kisha unampa mifano iliyopo wazi kisha unatumia nafasi kuwa unaweza kummunganisha na idadi kubwa ya watu wasiofahamu bidhaa yake.
Usiwe msemaji sana bali pia bidii ya matendo ni muhimu ile ufanikiwe kwani kupata wateja si muujiza tu bali pia mikakati makini.
Kutangaza unaweza kutumia tovuti yako rasmi, redio, facebook, group za whatsapp, instagram, magari ya matangazo, matamasha mbalimbali, kumbi za burudani, sherehe mbalimbali, mabango ya barabarani, vipeperushi, n.k.
Jinsi ya kufanikiwa
Jenga mawasiliano mazuri na wazalisha bidhaa na uwape madokezo unayopata unapotangaza bidhaa na ukumbuke kufanikiwa kwao ndio pia kufanikiwa kwako