Mahali
Mahali pa kufanyia biashara ni eneo lolote lenye watu wengi na hauhitaji fremu, mahali hapo panaweza kuwa jirani na soko, maeneo ya kituo cha mabasi, shuleni, vyuoni, ufukweni au eneo lenye wapitaji wengi.
Ujuzi
Ujuzi unaotakiwa ni kuchoma mishikaki mitamu kwa kuchanganya viungo vyote vinavyohitajika pamoja na jinsi ya kukata vyama vipande na bei yako(200 inafaa sana kwa kuanzia)
Kama huna ujuzi usiogope tembea youtube kuna mafunzo mengi ya kutengeneza mishikaki mitamu na viungo vyote vinavyohitajika.
Mahitaji
- Tatufa jiko(Nenda sehemu wanapochomelea unaweza kuongea nao vizuri jiko linapatikana ukiwa na 23000Tsh).
- Pata nyama isiyo na mifupa(StekiKwa kuanza na kilo 2 Bei ya kilo ni 8000Tsh maeneo mengi).
- Mkaa(Kupo tatu ni 1500TSH).
- Viungo vyote vinavyohitajika(Makadirio ni 5000).
- Vijiti vya mishikaki(2500Tsh).
Kwenye 2kg unaweza pata faida ya 10,000TSH baada ya kutoa matumizi yako vyote.
Na biashara umeanza kwa mtaji wa 23000+8000X2+1500+5000+2500=48000 tu.
Note:Ukataji wa vipande unahakisi faida, mfano tuseme ili upate faida ya 10000Tsh lazima upige hesabu.
Hesabu ya kulenga faida kwenye mishikaki ipo kwenye vipande, sasa ili kujua vipande unavyotakiwa kukata:
vipande=(mtaji+faida unayolenga)/(bei ya kipande)
mfano kwa kilo 2(mtaji=48,000, faida nayolenga ni 10,000 kipande nauza 200)
vipande=(48,000+10,000)/200
vipande=290
Kwa hivyo ili kupata faida ya 10,000 kwenye 2kg ya steki natakiwa nikate vipange 290.