Nyanya ni mojawapo ya viungo muhimu sana katika mapishi.Bila shaka karibu kila siku tunakula vyakula vilivyoungwa kwa nyanya.
Lakini kutokana na ukulima duni, usafirishaji na usindikaji duni nchini bado kuna kiwango kikubwa cha uingizaji wa viungo vya nyanya(tomato paste) licha ya kuwepo na wakulima wa nyanya wakutosha nyanya nyingi zinaribika kuliko zinazowafikia watumiaji.Wakati wa mavuno nyanya huzidi sana sokoni na kuuzwa bei ndogo sana lakini mara nyanya huadimika na kuwa ghali mno au kukosekana kabisa.
Hii inakupa fursa ya kuanzisha kiwanda kidogo tu na kufaidika sana na idadi ya watu inaongezeka kwa kasi sana ripoti ya UN inaonyesha barani Afika pekee idadi ya watu waishio mjini inataongezeka kutoka 414Million kwa sasa hadi 1.2billion mwaka 2050 soko zuri sana.Ongezeko hilo ni pamoja na uhitaji mkubwa wa vitu vya kila siku kama nyanya.
Kuna wataalamu wengi wausindikaji na ni rahisi sana kwa ukitumia mbinu za kuvutia
watumiaji kama kuongeza baadhi ya viungo katika product zako za tomato paste.Hivyo hii ni biashara muhimu na uhakika wa soko ni mkubwa.
Tunde Felix Ogunde mwanzilishi wa QSR Consult(Nigeria) alianzisha ukulima na usindikaji wa nyanya na usindikaji kwa miaka miwili tu biashara ilifika dola 200,000/=(sawa 400milionTsh).
Usisahau kulike facebook page yetu/tufuate twitter kupata mawazo zaidi