DONDOO MUHIMU KUANZISHA BIASHARA YA KUKU WA KIENYEJI.
- HAkikisha una eneo la kutosha kujenga banda na sehemu ya wazi.
- Hakikisha unajenga banda imara na limeezekwa vizuri (fuata utaalamu wa kujenga kama kuna upepo upe kisogo)
- nunua mashine ya kuangulia mayai incubator(inauzwa kutokana na idadi ya mayai inayoangua)
- tafuta mayai yenye mbegu na tumia mashine kuangua
- tunza vifaranga vyako kwa utaalamu na kuku wa kienyeji wanahitaji sehemu ya wazi yenye udongo hukua haraka.
- unaweza kuuza vifaranga kwa wafugaji wadogo ama kuwakuza mwenyewe.
- Hakikisha unapata mtaalamu wa mifugo kwa chajo na dawa za magonjwa mbalimbali
tafuta soko la kuku wako na unaweza uza kwa jumla ama rejareja